3 Septemba 2025 - 23:37
Source: Parstoday
Spika wa Iran: Waislamu wana wajibu wa kukomesha mauaji ya Israel Gaza

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameyataka mataifa ya Kiislamu kuungana katika vita dhidi ya utawala wa Kizayuni, ambao ameutaja kuwa shetani mkubwa zaidi duniani.

Akitoa hotuba yake katika kikao cha wazi cha Bunge la Iran leo Jumatano, Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Qalibaf amesema: Wiki ya Umoja na Maulidi ya Mtume Mtukufu (SAW) ni fursa ya kusoma tena ujumbe mkuu wa Uislamu, ambao ni udugu, maadili na uadilifu.

Ameeleza bayana kuwa: Kwa kuzingatia jina na kumbukumbu ya Mtume Mtukufu, taifa lolote la Kiislamu lazima lifungamane na umoja na mshikamano, na vile vile kuegemea umoja huo dhidi ya maadui.

Sanjari na kulaani vikali ukatili wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, Spika wa Bunge la Iran amesisitizia udharura wa kuchukuliwa hatua za haraka na za moja kwa moja za nchi za Kiislamu za kukomesha jinai hizo.

Spika wa Bunge la Iran amesisitiza kuwa, umoja huo si mbinu ya kisiasa, bali ni hitajio la kidini na la kistratijia kwa ajili ya heshima ya Umma wa Kiislamu na kuwashinda maadui.

"Waislamu wanapaswa kulaani jinai na mauaji ya kimbari huko Gaza kwa kauli moja na bila kigugumizi, na serikali za Kiislamu lazima zifuate wananchi na kuchukua hatua za kivitendo kukomesha mauaji ya Wazayuni," amesema Qalibaf.

Your Comment

You are replying to: .
captcha